KAMPUNI YA JAMBO YAANZA KUNUNUA ZABIBU KWA WAKULIMA DODOMA

Kampuni ya Jambo Food Products ya Mjini Shinyanga jana imeanza kununua zabibu kutoka kwa wakulima katika maeneo mbalimbali mkoani Dodoma ikiwa ni siku chache baada ya tamko la Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Mohamed Bashe alililotoa wakati akijibu changamoto za wakulima wa zabibu walizowasilisha mbele ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan aliposimama kuwasilimia eneo la Mpunguzi,Jijini Dodoma.

Zoezi la ununuaji wa zabibu katika mashamba ya Mpunguzi,Handali na Hombolo limeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Anthony Peter Mavunde ambaye pia alielezea mikakati mbalimbali inayofanywa na serikali kutatua changamoto hii;

-Kuongeza wigo wa masoko ya zabibu kwa Kampuni za Vinywaji nchini na nje ya nchi,Kwa sasa tunaishukuru sana Kampuni ya Jambo Ltd kwa kuanza na ununuzi wa Tani 3000 za zabibu kwa awamu hii,tunakaribisha wadau wengine pia watengenezaji wa vinywaji kuitumia zabibu yenye ubora kutoka Dodoma kama sehemu ya malighafi yao ya viwanda.

-Serikali imekaa na baadhi ya wamiliki wa viwanda vya uchakataji zabibu ili kuangalia uwezekano wa kupunguza mchuzi wa zabibu kwenye matenki yao ili ipatikane nafasi kwa ajili ya zabibu zilizopo mashambani.
*Kampuni ya CETAWICO imeshapunguza zaidi ya lita 250,000 kwenye matenki yake ya Hombolo na kuanza kuchukua mchuzi lita 30,000 katika matenki ya Ushirika wa Wakulima wa Zabibu Mpunguzi(UWAZAMAM) hali ambayo itawezesha kupatikana nafasi na kuhifadhi mchuzi wa zabibu utakaotokana na zabibu za msimu huu.

*Kampuni ya KISITU WINERY nayo ina nafasi ya uhifadhi wa mchuzi wa lita 200,000 na kwasasa tunashirikiana nao kwa kuzishirikisha Taasisi za kifedha ili na wao waweze kununua zabibu zilizopo mashambani.

-Kuangalia upya sera za kikodi ili kuufanya mvinyo kutoka Dodoma kuwa shindani kwenye soko la mvinyo nchini na kimataifa pia.

-Wizara ya Kilimo kutekeleza bajeti ya Ujenzi wa vituo vya uchakataji na uhifadhi wa mchuzi wa zabibu ili kunusuru zabibu za wakulima kuoza shambani pindi yanapotokea matatizo ya Soko.

Naye Mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Ndg. Emmanuel Ngusa amewahakikishia wakulima wa zabibu wa Mkoani Dodoma juu ya nia na dhamira ya Kampuni ya Jambo kuendelea kuwa soko la uhakika la zabibu baada kujiridhisha ubora

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *