FCS YATOA RUZUKU YA BILIONI 3.9 KWA AZAKI KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO TANZANIA BARA NA VISIWANI

Dodoma, 15 Agosti 2022. Shirika la Foundation for Civil Society (FCS) limetoa ruzuku ya shillingi 3,957,301,580 kwa asasi za kiraia (AZAKI) 89 Tanzania bara na visiwani kutekeleza miradi ya kimaendeleo chini ya programu za utawala bora katika sekta za maji, elimu, afya na kilimo; usawa wa kijinsia; ujumuishwaji wa vijana na watu wenye ulemavu, na ujenzi wa amani na mshikamamo wa kijamii kwa mwaka 2022-2023.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la foundation for civil society (FCS) Francis Kiwanga kushoto akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi 3.9 ikiwa na ruzuku kwa baadhi ya asasi za kiraia (AZAKI) kati ya 89 za Tanzania Bara na Zanzibar kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa na azaki hizo


Akizungumza katika warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI hizo zilizochaguliwa kupata ruzuku jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga alisema FCS imejitika katika kuhakikisha miradi inayofadhiliwa inawasaidia wananchi katika kuboresha maisha yao na kukuza sekta ya asasi za kiraia.
‘’FCS imepitisha mpango mkakati mpya wa mwaka 2022-2026 ambao unataka kuona wananchi waliowezeshwa, wastahimilivu, wanaowajibika na wanaopata haki za kiuchumi, kijamii na kuboresha ubora wa maisha yao. Tutaweza kufanikisha malengo yetu kwa kuchangia maendeleo endelevu na shirikishi nchini Tanzania kwa kuimarisha uwezo, kugawana rasilimali, na ushirikiano wa kimkakati na AZAKIi, vikundi vya jamii pamoja na watendaji wengine wa maendeleo,’’ alisema.
Edna Chilimo Meneja Programu Utawala Bora FCS alizugumzia ruzuku mbalimbali ambazo FCS imetoa kwa AZAKI ikiwemo ruzuku ndogo, za kati na ruzuku za kimkakati. Alieleza zaidi na kusema,

‘ Tunafanya kazi na mashirikia madogo sana ambao wabia wanafika na pia tunafanya kazi na viongozi wa klasta za programu wambao wanafanya kazi katika ngazi ya taifa. Tunafanya kazi na asasi za Kijiji, kata na wilayani. Wabia na mashirika tunayofadhili ni wadau muhimu ili wawafikie wananchi waweza kuleta mabadiliko na maendeleo . Mashirika yanayofadhiliwa na FCS sio Waruzukiwa tu, ni wabia pia. Baadhi ya Misingi ya ubia ni uelewa wa pamoja,malengo ya pamoja, na kuaminiana ili tuweze kufikia malengo ya pamoja. Tunajengea uwezo Azaki ili ziweze kutekeleza miradi vizuri ,kuweza kujiongoza, iwe imara na inayotambulika. Tunajengea uwezo Azaki ili kuweza kuandaa na kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali, Sekta binafsi, Mwananchi na Azaki nyingine. Tumekuwa Walezi wa sekta ya AZAKI. Tumechangia ukuaji wa sekta, miaka ya nyuma tulitoa fedha kwa Azaki kujisajili na sasa kuna Azaki zimekua, kutoka shirika dogo hadi kuwa mashirika makubwa yenye sifa. “Maadui wakubwa watatu wa maendeleo ni Umaskini, ukosefu wa haki (injustice), hali ya kutenga na kubagua wengine. Mdau mkubwa na maendeleo ni Mwananchi mwenyewe aliyewezeshwa ,anaejitambua, wenye ustaimilivu na mwenye sauti ili aweze kuleta maendeleo yake”

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la foundation for civil society (FCS) Francis Kiwanga kulia akishuhudia afisa programu wa shirika la wanawake katika sheria na maendeleo barani afrika WILDAF Vera Assenga akisaini mkataba wa kupokea ruzuku iliyotoleea na FCS kwa ajili ya kusadia miradi ya kimaendeleo katika hafka iliyofanyika leo dodoma FCS imetoa jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 3.9 kwa asasi 89 za tanzania bara na Zanzibar

FCS ni shirika huru la maendeleo, la Kitanzania lisilolenga kupata faida, ambalo hutoa ruzuku na huduma za kuzijengea uwezo asasi za kiraia nchini Tanzania. Tangu kuanzishwa kwake miaka 20 iliyopita FCS imechangia kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha uwezo wa sekta ya kiraia nchini Tanzania. FCS imeziwezesha asasi za kiraia chachu ya maendeleo na wananchi kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha utawala wa kidemokrasia nchini Tanzania. Juhudi hizi zinalenga kuboresha utoaji wa huduma, hasa katika ngazi za chini za jamii na hatimaye kuboresha maisha kwa wote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *