KUELEKEA UTIAJI SAINI MIKATABA KATI YA TARURA NA MAKANDARASI WATAKAOTEKELEZA KAZI ZA UJENZI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23

  1. Serikali ya Awamu ya Sita imeongeza bajeti ya kaz za Ujenzi, Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kutoka TZS bilioni 272.56 mwaka 2021 hadi kufikia TZS bilioni 722.22 mwaka 2021/22 na kufikia TZS bilioni 776.63 kwa fedha za ndani sawa na ongezeko la 185%.
  2. Kufuatia ongezeko la Bajeti hali ya mtandao wa barabara zinazosimamiwa na TARURA wenye km 144,429.77 umeimarika ambapo barabara za lami zimeongezeka kutoka km 1,449.55 hadi km 2,635.75 sawa na ongezeko la kilomita 1,186.2 ambazo ni ongezeko la 81.8%. Aidha barabara zenye hali nzuri na wastani (good and fair) imeongezeka kutoka kilomita 61,867.47 hadi kilomita 82,740.36 sawa na ongezeko la kilomita 20,872.89 ambazo ni ongezeko la 33.74%.
  3. Ofisi ya Rais – TAMISEMI iliona ni vyema kuweka mikakati ya kuhakikisha fedha zinatumika kwa wakati hivyo ilielekeza TARURA kuanza taratibu za manunuzi mapema mara tu baada ya bajeti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuidhinishwa na Bunge. TARURA ilitangaza kazi zenye thamani ya TZS bilioni 378.56 sawa na asilimia sitini (60%) ya fedha za ndani zilizopangwa kutekeleza miradi ya barabara.
  4. Miradi iliyo tayari kusainiwa ni 968 yenye thamani ya TZS bilioni 248.74 na miradi 117 yenye thamani ya TZS bilioni 129.83 imetangazwa upya baada ya Wakandarasi walioomba kutokidhi vigezo.
DCIM\100MEDIA\DJI_0028.JPG
DCIM\100MEDIA\DJI_0188.JPG

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *