Mbunge wa ushetu mkoani Shinyanga Mhe.Emmanuel Cherehani amewaomba wananchi wa Jimboni kwake kuwekeza nguvu zao katika kilimo na sio kutumia muda wao mwingi katika kucheza mchezo wa karata

Akizungumza Leo jimboni kwake Ushetu,Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kwenye kongamano la kuhamasisha Sensa na Kumpongeza Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan Kwa kuweka ruzuku ya mbolea Kwa wakulima,Mhe.Cherehani amesema wananchi hao wa ushetu ni vyema wakawekeza nguvu zao katika kilimo na kuacha kucheza karatu kwani Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassani ametoa fedha zipatazo bilioni 28 kwa ajili ya Ruzuku ya Mbolea Kwa wakulima
“Mhe.Rais ametoa ruzuku ya mbole kwa wakulima wa ushetu bilioni 28 twendeni tukalime tuache kucheza karata”amesema Mhe.Emmanuel Cherehani
Mhe.Chereheani amesema kitendo Cha Rais Mhe.Samia kuweka ruzuku hiyo ya Mbolea kwa wakulima inakwenda kuwasaidia wakulima wa ushetu ambao wamekuwa wakinunua ngunia Moja la mbolea Kwa shilingi 140000
Na Fadhili Komba
Picha za Matukio ya kongamano la kuhamasisha Sensa na Kumpongeza Rais




