DAWASA YAANIKA MIKAKATI YA KUMALIZA KERO YA MAJI DSM KWA ASILIMIA 100

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja,akizungumza na waandishi wa habari  leo Agosti 13,2022 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2022-2023.


Mamlaka ya amaji safi na usafi wa mazingira Dar es salaam(DAWASA) imesema inatekeleza miradi13 ya kimkakati yenye thamani ya Tsh Trion 1 na Milioni 60 kwa mwaka, huku bajeti ya fedha ya mwaka hikiwa ni sawa na Tsh Bilion 162.
Hayo yamesemwa na Mhandisi Cyprian Luhemeja Afisa mtendaji mkuu (DAWASA) leo jijini Dodoma wakati wa Uwasilishaji wa taarifa ya utekerezaji wa miradi katika mamlaka hiyo ambapo amesema lengo la (DAWASA) kufikia mwaka 2023 nikufikia asilimia 100% kwa kusambaza maji safi.
Aidha Mhandisi Luhemeja mesema katika jiji la Dar es salaam yapo majimbo ambayo yamekwisha sahau changamoto ya maji kwa kupata maji kwa asilimia 100% majimbo hayo ikiwa ni pamoja na jimbo la Ilala, na Ubungo huku jimbo la Kawe na Kigamboni yakitarajia kupata huduma ya maji kwa asilimia 100% ifikapo Desemba mwaka huu.
“Lengo la (DAWASA) kufika mwaka 2023 nikufikia asilimia 100% kwa kusambaza maji safi, na asilimia 60% kwa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira Pia tunaendelea kutekeleza miradi ya kimkakati 13 yenye thamani ya Tsh Tirion 1 na miliono 60.
“ Yapo majimbo ambayo yamesha sahau changamoto ya maji kwakupata maji kwa aslilimia 100% Majimbo hayo ni Ilala na Ubungo na tunatarajia mpka kufika desemba mwaka huu jimbo la Kawe na Kigamboni pia yatakuwa yanapata maji kwa asilimia 100%”alisema Mhandisi Luhemeja.

Na Johndickson Gaudin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *