MATAMASHA SIMBA DAY, WIKI YA MWANANCHI NA TASWIRA DABI YA KARIAKOO

Na Editha Chiwaligo

Wahenga wanasema hayawihayawi sasa yamekuwa. kilele cha siku ya mwananchi ambayo imefanyika tarehe 6 Agosti mwaka huu siku ya jumamosi katika uwanja wa Benjamini mkapa ambapo kulikuwa na maonyesho mbalimbali ikiwemo kuwepo kwa wasanii waliopanda jukwaani kwaajili ya kutoa burudani mbalimbali hii yote kwaajili ya kusherehesha siku yao .

 Bila kusahau pia yanga waliweza kutambulisha wachezaji wao wapya walio sajiliwa kwaajili ya msimu ujao. Ambao msimu huo utafunguliwa tarehe 13 Agosti mwaka huu. Ambayo siku hiyo watakichapa dhidi ya Simba Sports Club dhidi ya watani wao wa jadi Young Africa.

Katika siku ya wananchi kulikuwa na michezo mbalimbali ambapo Young princess alicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ilala Queens, ambapo Yanga princess ilitoka na mabao manne kwa sifuri katika mchezo wao wa kirafiki. Bila kusahau pia Young Afrika waliweza kucheza na Vipers ambapo yanga ilifungwa mabao mawili kwa sifuri katika uwanja wao wa nyumbani.Hakika siku hiyo ilikuwa ni siku ya kihistoria kwa wachezaji pamoja na mashabiki.

wanasema kwamba mcheza kwao hutunzwa, nazungumzia kilele cha siku ya simba yaani Simba day ambayo imefanyika tarehe 8 Agosti mwaka huu [NANENANE] katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam. katika siku hiyo kulikuwa na shamlashamla pamoja na matukio mbalimbali ambayo yaliweza kuipamba siku hiyo. 

Aidha katika siku hiyo yaani Simba day kulikuwa na maonyesho mbalimbali ambapo mashabiki wa simba waliweza kujaza uwanja wa Benjamini mkapa mapema sana hii yote inaonyesha ni jinsi gani mashabiki pamoja na wachezaji wanavyo ithamini siku yao na jinsi walivyo ipania kuonyesha utofauti na sikukuu zilizo pita.

Pamoja na hilo kulikuwa na tukio la watoto walio onyesha Alaiki watoto hao waliingia uwanjani na kuonyesha maumbo mbalimbali yalio someka kama, ASANTE WANA SIMBA, ASANTE MO DEWJI, NGUVU MOJA  hii yote ni katika kuhakikisha kuwa simba day inakuwa ni siku ya kipekee na yakitofauti.

pia palikuwa na wasanii mbalimbali waliweza kutumbuiza katika jukwaa ikiwemo msanii mwanadada Zuchu ambae aliweza kushangaza wananchi wengi sana uwanjani kwa jinsi alivyo ingia katika uwanja wa Benjamini Mkapa kwa jinsi alivyoshuka na kamba kutokea juu kabisa kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa mpaka kutua katika uwanja huo na kuanza kutumbuiza. kwakweli ilikuwa ni jambo la kihistoria kwa mwanadada huyo kwa namna jinsi alivyo washangaza watu katika uwanja huo.

Sambamba na hayo simba sport club waliweza kutambulisha wachezaji wao wapya walio sajiliwa kwaajili ya msimu ujao ambao msimu huo utafunguliwa tarehe 13 Agosti mwaka huu. pamoja na hilo mashabiki pamoja na wachezaji wakiwa wanausubiri kwa hamu mchezo utakao chezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Benjamini mkapa . Ambapo simba sport club watakiwasha pamoja na Young Africa ngao ya jamii.

Aidha haikuishia hapo palichezwa mechi ya kirafiki kati ya Simba Queens dhidi  ya Fountain Gate Academy kikosi cha wanawake kutokea Dodoma ambapo mechi hiyo ilikuwa kali sana ambapo Simba Queens waliweza kujiondokea na mabao mawili kwa sifuri katika uwanja wao wa nyumbani.

Zaidi ya yote mechi kubwa sana iliyokuwa inasubiliwa kati ya Simba Sport club pamoja na St. George kutokea Ethiopia ambapo mechi ilichezwa saa 1 jioni mechi ambayo mashabiki wa simba waliisubiri kwa hamu sana ili kujionea wenyewe wachezaji wao wapya walio tambulishwa kwaajili ya msimu ujao kwamba yaliyomo yamo??

Simba Sport club dhidi ya St.George kutokea Ethiopia mchezo ulikuwa mgumu sana lakini simba sport club ili kuiweza kuipamba vizuri siku yao waliweza kujiondokea na mabao mawili kwa sifuri katika uwanja wao wa nyumbani Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam hakika kikosi cha Simba kilikuwa kikali sana.

Hii yote ni katika kuonyesha utofauti wa sikukuu hizi mbili ambapo tumeweza kuona ni jinsi gani timu hizi zote mbili zilivyo weza kufanya ubunifu mbalimbali hususa kikosi cha simba kilivyo weza kufanya maonyesho mbalimbali katika sikukuu yao. Pia Pande zote viliweza kutambulisha wachezaji wao wapya pamoja na kuonyesha ufanisi mkubwa katika uwanja na hii inaonyesha ni jinsi gani vikosi vyote viwili vilivyo weza kujiandaa tayari kwaajili ya mechi ijayo ya Ngao ya hisani ambapo mara ya mwisho katika Kombe hili magwiji hawa walipokutana Young Africa iliweza kujiondokea na bao moja kwa sifuri  aliloweza kufungaMshambuliaji hatari wa KIkongo Fiston Mayele.

Sasa swali la kujiuliza je, ni nani atakae weza kuibuka kidedea katika mechi  hiyo? Mtanange mkali wa watani hawa wa jadi kati ya Simba Sport Club dhidi ya Young Africa, utakaochezwa siku ya jumamosi tarehe 13 Agosti mwaka huu  Majira ya Saa Moja Jioni pale katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijijni Dar es salaam.

Yanga wakitamba na nyota wao akiwemo Bernad Morrison aliyerejea akitokea Simba, Aziz Ki, Gael Bigirimana, na wengine wengi. Wakati Simba wao wakitamba na Wachezaji kama Augstine Okrah, Nelson Okwa, Clatous Chama na yule mzungu kutoka nchini Serbia Pamoja na wengine wengi.

Macho na Masikio nip alee kwa Lupaso.je ni Yanga tena ama Mnyama?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *