Na Johndickson Gaudin
Wakati Dunia na wanakenye wakiendelea kusubilia uamuzi wa matokeo ya kura ya Uraisi nchini Kenya hali imeendelea kuwa tulivu huku baadhi ya maeneo yakiwa yamekwisha kumaliza mchakato mzima wa uhesabuji kura na kufanya baadhi ya vyombo vya habari vya nchini humo kuanza kutangaza matokeo ya majimbo mbalimbali
Kwamujibu wa chombo cha habari cha Citizen cha nchini humo kimeeleza kuwa hadi sasa matokeo ya urais yanayo endelea kutangazwa Bw Willliam Ruto ameendeleo kuongoza katika maeneo ya Bonde la Ufa na maeneo ya Mlima Kenya Huku mwenzake Bw Raila Odinga akiongoza katika maeneo ya Nyanza Nairobi pamoja na maeneo ya mashsriki na pwani
Aidha chombo hicho kimeonyesha Bw Ruto amendelea kuongoza kwa wingi wa kura hakiwa na asilimia 50.3% na huku Bw Odinga kuwa na kura sawa na asilimia 48.46%
Uchaguzi huu wa mwaka 2022ni uchaguzi wa awamu ya Tano na unajumuisha wagombea wa Urais wanne ambao ni William ruto , Laila Odinga, Prf George Wajackoyah na Devid Mwaure na hadi sasa wagombea wawili ndo wanao onekana kuwa na mchuano mkali katika kinyanganyiro hicho cha kiti cha Urais.
Ikumbukwe kuwa wagombea wote wa Urais waliweza kutimiza jukumu lao la kikatiba katika maeneo yao waliyo andikishwa kwaajili ya kupiga kura hapo jana na ripoti katika vyombo mbaalimbali kutoka nchini humo vimeleza kuwa hali ya Amani nchini humo iko salama hadi sasa wakati matokeo yakiwa yanaendelea kutangazwa katika maeneo mbalimbali