HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA YAWAKUMBUKA WAKULIMA KWA KUTOA HUDUMA YA AFYA NANENANE

Hospitali ya Benjamini mkapa ya Jijini Dodoma leo agasti 8,2022 imeshiriki katika maadhimisho ya Sikukuu ya wakulima(nane nane) ambapo imetoa huduma mbalimbali za afya na elimu ya mtindo wa maisha pamoja na upatikanaji wa Bima ya Afya kwa wakulima ambazo sitaweza kuwasaidia kupatiwa matibabu

Akizungumza Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt.Alphonce Chandika, Msemaji wa Hospitali hiyo Jeremiah Mbwambo amesema kushiriki Kwa Hospitali hiyo katika maadhimisho hayo ni namna ambavyo Hospitali hiyo itakavyoweza kitumia siku hiyo kukutana na wakulima ili kuwapatia huduma ya afya na elimu ya upatikanaji wa Bima ya afya.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya dharula Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt.George Dilunga amesema kilimo ndio Uti wa mgongo wa Taifa na kama wakulima hawatakuwa na afya njema itasababishaTaifa kukubwa na balaa la njaa hivyo wao kama wataalamu kutoka hospitali hiyo wameona ni vyema kushiriki maadhimisho hayo ili kutoa huduma hiyo Kwa wakulima.
“Wakulima kama tunavyojua ndio uti wa mgongo wa Taifa letu na wao ndio sehemu kubwa ambayo bila kuwa na afya njema basi ina maana kwamba kilimo cha Nchi yetu hakitafanikiwa”amesema Dkt.George Dilunga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *