WAZIRI MKUU AZINDUA VITABU VYA KIMKAKATI ELIMU MSINGI NA SEKONDARI

OR-TAMISEMI

Pamoja na Ufunguzi wa Mashindano ya UMITASHUMNTA na UMISSETA, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezindua vitabu vitatu vya kimkakati vya kutoa miongozo na mikakati ya kuboresha Elimu Msingi na Sekondari nchini pamoja na kuimarisha uongozi katika Ngazi za Shule, Kata, Halmashauri pamoja na Mikoa.

Vitabu hivyo vimezinduliwa rasmi katika Ufunguzi wa mashindano ya michezo katika Shule za Msingi (UMITASHUMNTA) pamoja mashindano ya michezo katika shule za Sekondari (UMISSETA) tarehe 04 Agosti 2022 Mkoani Tabora.

Akisoma taarifa yake Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde amesema kuwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI iliunda kikosi kazi kilichobainisha changamoto zote za uendeshaji wa Elimu ya Msingi na Sekondari pamoja na kutoa muongozo wa nini kifanyike ili kuboresha elimu nchini.

“Kipitia uchambuzi huo uliofanywa na kikosi kazi hiko Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeandaa vitabu vitatu vitakaotoa miongozo na mikakati ya kuboresha Elimu Msingi na Sekondari nchini pamoja na kuimarisha uongozi katika ngazi za Shule, Kata , Halmashauri na Mikoa nchini” Mhe. Silinde

Akivitaja vitabu hivyo Mhe. Silinde amesema kitabu cha kwanza kinaitwa muongozo wa uteuzi wa viongozi wa elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa ,
amebainisha kuwa kitabu hicho kimeanisha taratibu zinazopaswa kuzingatiwa katika kuteua viongozi wa elimu ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa ili kuwawezesha waliopewa dhamana ya uteuzi kurejea taratibu za kufuata wakati wa uteuzi wa viongozi wa elimu.

“Kitabu cha pili kinaitwa Changamoto katika uboreshaji wa Elimu Msingi na Sekondari na nini kifanyike, kitabu hiki kimebainisha changamoto kuu za utekelezaji wa maboresho ya ufundishaji na ujifunzaji pamoja na hatua vinavopaswa kuchukuliwa na viongozi wa elimu kutoka ngazi zote kuanzia ngazi ya shule hadi Taifa” Mhe. Silinde

Cha tatu ni kitabu cha kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi ya elimu msingi, amesema kuwa kitabu hiki kimelenga kuwawezesha wataalam na walimu kubaini changamoto za kina za ufundishaji na ujifunzaji zilizopo, athari za changamoto hizo, fursa zilizopo pamoja na kutumia mikakati ya utatuzi wa changamoto hizo.

“Vitabu hivi vya kimkakati vimelenga kila msimamizi wa elimu Msingi na Sekondari kuhakikisha anazidisha ubunifu na uweledi katika ufundishaji mwenye kuleta tija inayotarajiwa kwa mwanafunzi mmoja mmoja kwa kutumia mbinu mbalimbali zikiwemo michezo na Sanaa za Maonesho” Mhe. Silinde

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *