WAZIRI JAFO ATOA MAAGIZO KWA MKURUGENZI DODOMA NA DUWASA

Soko la Bonanza Dodoma lapongezwa kwa usafi wa mazingira unaofanywa sokoni hapo na kutumika kama soko la kuigwa na masoko mengine jijino hapo na nchi nzima.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Muungano na Mazingira Dr Suleimani Jafo alipotembelea soko hilo katika kampeni ya utunzaji wa mazingira iliyoandaliwa na mabarozi wa usafi katika soka hilo kwa lengo la kuendeleza kampeni ya kufanya usafi kwa kila jumamosi.

Dr Jafo amesema ameridhishwa na usafi unaofanywa kwenye soko hilo na kuitaka mikoa mingine pamoja na masoko nchi nzima kuiga mfano uliokuwepo katika soko la Bonanza na kuifanya Tanzania kua nchi inayosimamia usafi wa mazingira na kuigwa na nchi nyingine barani Afrika.

Aidha Waziri Jafo ameitaka mamlaka ya maji dodoma DUWASA kutatua changamoto ya mifereji ya na kutoa wiki moja.

Pia amemuagiza Mkurugenzi wa jiji na ofisi yake kuleta vifaa vya usafi katika soko Hilo na kutoa mwezi mmojia kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *