
Naibu Katibu Mkuu UVCCM Taifa- Bara, Ndugu Mussa Mwakitinya (MNEC) apokea taarifa rasmi ya Mafunzo ya Uongozi ya YALI- Mandela Washington Fellowship 2022 aliyoshiriki Ndugu Victoria Mwanziva Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM Taifa.
Taarifa hii inaelezea mafunzo ya YALI- MWF na mrejesho mzima wa ushiriki wake na namna ambavyo taasisi na vijana wa Chama Cha Mapinduzi wanaweza kunufaika na uwakilishi huu, na namna ya kuziendea fursa mbalimbali za Kimataifa.
