AWESO AZITAKA BODI ZA MABONDE YA VYANZO VYA MAJI ZISIMAMIE SHERIA

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Hamidu Aweso ametembelea Bonde la Ziwa Victoria mkoani Mwanza,
Akiwa katika Bonde hilo amekagua kituo cha kuchukulia takwimu za kina cha maji ya ziwa victoria kwenye kituo kilichopo Mwanza south na kujionea usafi wa ziwa na jinsi Bodi inavyoondoa gugumaji
Pili amekagua teknolojia mpya ya kupokea takwimu za maji na kuona namna zinavyochakatwa hadi kupata taarifa yenye kueleweka kwa urahisi zaidi kwa wadau.
Aidha Waziri Aweso amezindua Bodi ya saba ya Bonde la Ziwa Victoria na kukabidhi vitendea kazi kwa Bodi hiyo.

Katika hatua nyingine akizungumza na watumishi wa Bonde la Ziwa Victoria amesisitiza kuwa maji ni uhai, maji ni bidha ya kiuchumi, maji hayana mbadala ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha analinda, anatunza na anahifadhi vyanzo vya maji kwa maendeleo endelevu. Hivyo, ameagiza Bodi za maji nchini kusimamia sheria na kuchukua hatua kwa wale wote wanaovunja sheria ikiwa ni pamoja na wale wanaochimba visima bila vibali, wanaofanya shughuli za kibinadamu kwnye hifadhi ya vyanzo vya maji na wale wanaotumia maji bila vibali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *