Prof. Shemdoe awafunda Makatibu Tawala & Wakurugenzi

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe ametoa wito kwa Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi kuendelea kusimamia vyema majukumu ya kazi kwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za kazi walizopewa.

Prof. Shemdoe amesema hayo Julai 27, 2022 wakati akifungua kikao kazi cha kujadili Mwenendo wa Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani ya Halmashauri na Utekeleza wa Taarifa za Ukaguzi Maalum ulifanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Amesema malengo ya Serikali ni kuona Halmashauri zinafanya kazi zake kwa weledi na kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato

“Tufanyeni kazi kwa kujua kuwa malengo ya Serikali ni kuwahudumia wananchi wake sisi, viongozi tushirikiane kwa kuhakikisha Serikali inatimiza malengo yake kwa kutoa huduma kwa wananchi wake lakini pia ni kwa usimamizi wetu sisi tuliopewa dhamana katika Halmashauri zetu kuzisimamia” Prof. Shemdoe

Kwa upande wake Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Charles Kichere ametoa wito kwa viongozi hao kuendelea kuzijua na kuzifuata Sheria za ukaguzi lakini kutoa ushirikiano kwa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuweza kutekeleza majukumu yake ya Kisheria.

“Tuendelee kushirikiana ili tufikie malengo ya Serikali jukumu letu kubwa ni kuhakikisha Sheria, Kanuni na Taratibu zetu zinafuatwa” Kichere

Kikao kazi hicho cha lengo la kujadili Mwenendo wa Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani ya Halmashauri kwa Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi kitahitimishwa Julai 29, 2022 kwa watendaji hao pamoja kwa kujadiliana, kutoa maoni, ushauri na muelekeo wa utekelezaji wa majukumu yao ya kazi katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na malengo ya Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *