
Bodi ya Wakurugenzi ya Ranchi za Taifa NARCO imetembelea Ranchi ya Ruvu iliyopo katika mkoa wa Pwani. Mwenyekiti wa Bodi ya NARCO Mhandisi CYPRIAN LUHEMEJA amesema NARCO inatarajia kutoa muongozo mpya wa utendaji kazi utakaoiwezesha kampuni hiyo ya Ranchi za Taifa kutekeleza majukumu yake kwa tija na kutoa mchango mkubwa kwenye pato la Taifa.
