Zanzibar.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mikoa ya Kaskazini na Kusini Unguja, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), leo Julai 26, 2022 ameshiriki matembezi na kuzindua Bonanza la Michezo la uhamasishaji wa Sensa ya Watu na makazi katika Jimbo la Nungwi Zanzibar lililofanyika katika Viwanja vya Vidimni.






