NARCO YABADILI MFUMO WA UFUGAJI RANCHI YA TAIFA WEST KILIMANJARO

Kampuni ya Ranchi za Taifa – NARCO imebadili mfumo wa ufugaji katika Ranchi ya Taifa ya West Kilimanjaro kwa kuifanya kuwa Ranchi pekee ya ufugaji wa Kondoo ili kukidhi mahitaji ya soko la Afrika Mashariki na kati.

Bodi ya Wakurugenzi ya NARCO ikiongozwa na Mwenyekiti wa bodi hiyo Mhandisi Cyprian Luhemeja imefikia hatua hiyo baada ya kutembelea Ranchi hiyo na kujionea makundi makubwa ya kondoo huku kukiwa na uhitaji wa mifugo hiyo katika viwanda vya nyama katika nchi jirani.

Bodi hiyo ipo katika ziara ya kutembelea Ranchi za Taifa zinazomilikiwa na NARCO ili kuongeza tija na mabadiliko katika sekta ya mifugo ili kukidhi soko la ajira na la mifugo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *