DKT. MAGEMBE AWAJULIA HALI WANAFUNZI WA KING DAVID

Naibu Katibu Mkuu Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa , Dkt. Grace Magembe ametembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula kuwajulia hali wanafunzi wa Shule ya Msingi King David ambao wamepata ajali mapema leo tarehe 26 Julai 2022.

Wanafunzi hao wanaendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo na hali zao zinaendelea kuimarika.

Aidha Dkt. Magembe anatoa salam za pole kwa wazazi ndugu na Jamaa ambao wameondokewa na watoto wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *