MARUFUKU UGAWAJI VITALU RANCHI YA MWISA ll WILAYANI MULEBA

Bodi ya Wakurugenzi ya Ranchi za Taifa – NARCO imezuia ugawaji wa vitalu katika ranchi ya MWISA II iliyopo Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa – NARCO Mhandisi CYPRIAN LUHEMEJA ameiambia kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Muleba ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Toba Nguvila kuwa Ranchi ya MWISA ll inatengwa ili kuwa kituo maalum cha kuhifadhi mifugo inayonunuliwa kwa wananchi kwa ajili ya kusafirishwa kwenda kwenye Ranchi za kunenepesha ili kukidhi masoko ya ndani na ya Kimataifa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Muleba Toba Nguvila amepongeza hatua zinazochukuliwa na NARCO na kuahidi kutoa ushirikiano ikiwemo wa ulinzi ili kuhakikisha ranchi hiyo linaleta manufaa kwa Taifa na wananchi wanaoizunguka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *