“HATUTOKUBALI KUONGEZA MUDA KWA MKANDARASI KIGOMA, KAZI IKAMILIKE KWA WAKATI ” WAZIRI AWESO

Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso amefika na kutembelea Eneo la Chanzo Cha Maji katika Mradi Mkubwa wa Maji Kigoma Mjini.
Mradi unatarajiwa kuzalisha lita milion 42 huku mahitaji ya maji yakiwa ni lita milioni 23 ambapo kata zote 19 za Mji wa Kigoma zimekwishakufikiwa na mtandao wa Bomba Kuu.

Akiwa eneo la mradi amekiri kuwa kazi kubwa ya Utekelezaji imeshafanyika na kumsisitiza Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji Kigoma kufanya kazi kubwa ya kuwaunganishia wananchi maji kwa maeneo yaliokwishafikiwa na mtandao wa Maji eneo la kilomita 53 na kugusa maeneo yote ya kata 19.

Aidha, Waziri Aweso amemsisitiza mkandarasi kukamilisha kazi yake ya Ujenzi wa Chanzo ndani ya miezi mitatu kama ilivyopangwa na kumueleza kuwa hataruhusu kuongezewa muda wa kuendelea na kazi baada ya mkataba kumalizika na kumtaka afanye kazi usiku na mchana mradi ukamilike ili wana Kigoma wakabidhiwe mradi wao.

Katika hatua nyingine Waziri wa Maji Aweso ametembelea eneo la Kamala Mlimani ambapo pamoja na uwepo wa kilima kirefu amelifika eneo hilo ambalo ni sehemu ya maeneo yaliyonufaika wa Mradi mradi huu na kupongeza kazi nzuri iliyofanika. Pia, ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni mia mbili kwa ajili ya ujenzi wa tanki lenye ukubwa wa lita laki tatu ktk eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *