
Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu, Simon Sirro amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe huku akisema ataitumikia nafasi hiyo kwa manufaa ya Taifa kama atakavyoelekezwa na mkuu wa nchi.
Balozi Simon Sirro ameyasema hayo katika Kijiji cha Muryaza wilayani Butiama mkoani Mara wakati wa Misa ya Shukrani kwa kulitumikia jeshi la polisi kama mkuu wa keshi hilo na kuteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.

Katika hafla hiyo ya shukrani Balozi Sirro amewaomba watanzania kumuunga mkono IGP mpya Camillus Wambura ili kuhakikisha jeshi hilo la polisi linafanya kazi yake ya kulinda raia na mali zao bila kikwazo chochote.
Balozi Sirro ametumia nafasi hiyo kutoa misaada mbalimbali kwa wananchi wa Butiama, yatima pamoja na maaskofu wa majimbo mbalimbali ya Mkoa wa Mara.
