Wakurugenzi endeleeni kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Raia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini waendelee kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo ili waweze kufanya shughuli zao kwenye maeneo rafiki bila bugudha yeyote.

Mhe. Bashungwa ameyasema hayo wakati akiongea na wafanyabiashara wadogo wadogo wa matunda na mboga mboga kwenye eneo la Mtumbati wilayani Kilosa nkoani Morogoro katika ziara yake ya kikazi Wilayani humo.

Amesema Wakurugenzi wanapaswa kutenga na kuboresha maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo kuendelea na shuguli zao katika mazingira bora na rafiki.

‘Niwapongeze uongozi wa Halmashauri ya Kilosa kwa kuboresha eneo la sokonla mtumbatu kwa ajili ya wafanya biashara hawa unaweza kuona namna ambavyo kwa sasa wanaweza kufanya biashara zao kwa masaa 24 kwa sababu mmewawekea Taa hivyo eneo hili linakuwa na mwanga wakati wote na magari hata yanayopita usiku wanaendelea kununua bidhaa za wajasiriamali hao’.

Aidha amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilosa kuendelea kutenga na kutoa mikopo kwa wajasariamali wakiwemo wafanyabiashara wa soko la hilo la mtumbatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *