
Bodi ya Ranchi za Taifa ( NARCO ) chini ya Mwenyekiti Mhandisi Cyprian Luhemeja imevunja mkataba na mwekezaji AGRO BUSINESS wa kitalu namba moja katika Ranchi ya Kitengule katika wilaya ya Karagwe mkoani Kagera baada ya eneo la kitalu hicho kutumika kusafirisha magendo ikiwemo ng’ombe na pembe za ndovu kwenda nchi jirani.
Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Karagwe ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Mwalimu Julieth Binyula amemueleza mwenyekiti wa bodi ya NARCO kuwa ilifanya uchunguzi na kubaini kampuni ya Agro Business haikuwa na mifugo katika ranchi hiyo na kuwa amewakodishia wafugaji wengine kwa gharama ya zaidi milioni 200 kwa mwaka.

Bodi ya Ranchi za Taifa ipo mkoani Kagera kukagua na kutembea ranchi mbalimbali zinazopatikana mkoani Kagera kwa lengo kurudisha Ranchi za Taifa katika ubora wake.
