WAZIRI AWESO ASHIRIKI MKUTANO WA INDIA NA NCHI ZA AFRIKA

Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso ameshiriki Mkutano wa 17 wa India na nchi za Africa – Confederation of Indian Industry Exim Bank Conclave unaohusu ushirikiano katika fursa za ukuaji wa kiuchumi baina ya India na nchi za Africa.
Mkutano huu ni fursa kwa nchi za Afrika na hususani Tanzania katika ukuaji wa mapinduzi ya Teknolojia, Vifaa na Vipuri mbalimbali vinavyotumika katika miradi ya sekta ya Maji.
Nchi ya India ni mdau mkubwa kwa sekta ya Maji nchini Tanzania

Mkutano huu umeudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Afrika ikiwa ni pamoja na Makamu wa Rais Zambia, Makamu wa Rais Gambia, Makamu wa Rais Mauritius, Makamu wa Rais Sudan, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje Namibia, na Mawaziri wa Maji toka nchi mbalimbali za Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *