WAZIRI MKUU AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI SINGIDA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 15, 2022 ameanza ziara ya kikazi mkoani Singida.

Mheshimiwa Majaliwa ameanza kwa kutembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Singida iliyopo katika kata ya Solya, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.

Ujenzi wa Shule hiyo ambao unatekelezwa kwa awamu mbili, utagharimu shilingi bilioni 4 mpaka kukamilika kwake, Halmashauri hiyo ilipokea shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kugharamia ujenzi katika awamu ya kwanza.

mradi huu utakapokamilika utawezesha wanafunzi 600 kutoka mkoa wa Singida kupata fursa ya elimu ya Sekondari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *