RAIS SAMIA ARIDHIA WADAIWA SUGU KODI YA ARDHI KUSAMEHEWA RIBA

SERENGETI JULAI 13, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameridhia kusamehewa riba ya kodi ya pango la ardhi kwa wadaiwa sugu kwa masharti kwamba wadaiwa hao wawe wamelipa madeni yq msingi ndani ya miezi sita kuanzia mwezi julai hadi desemba 2022.

Hayo yamebainishwa tarehe 12 Julai 2022 na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula katika mkutano na wananchi wa kijiji cha Nyachoka wilayani Serengeti mkoani Mara wakati wa zoezi la kukabidhi hati miliki za kimila.

Dkt Mabula alisema yeye pamoja na Waziri wa Fedha ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusamehe watakutana na kupanga namna bora ya kutekeleza msamaha huo.

“Najua kuna wengi wanadaiwa madeni ya muda mrefu kwa hiyo kumetokea msamaha kuanzia mwezi julai mpaka desemba mwaka huu, watakaoweza kulipa ndani ya miezi hii sita, wale ambao madeni yao yana miaka mitano kurudi nyuma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *