WAJUMBE BODI YA USHAURI TARURA WAENDELEA NA ZIARA UKAGUZI MRADI AGRI-CONNECT

Wajumbe ya Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) wameendelea na ziara ya ukaguzi wa barabara za Mradi wa Agri-Connect katika Mkoa wa IIringa, wilaya ya Mufindi na kukagua Barabara ya Sawala- Mkonge-Iyegeya yenye urefu wa kilomita 30.3.

Barabara hiyo imejengwa kwa thamani ya TZS . 8,167,087,887.00.

Lengo kuu la Mradi huu ni Kurahisisha usafirishaji wa mazao ya Mboga mboga, Chai, matunda na mazao mengine toka mashambani kwenda mikoa mingine au kwenda Viwandani ama katika maghala ya kuhifadhia.

Mradi huu pia umeleta faida nyingi za kiuchumi na kijamii, baadhi ya faida hizo ni:-
i. Upatikanaji wa Ajira kwa wananchi wanaoishi wa maeneo ya mradi wakati wa utekelezaji ambapo kiasi cha ajira 470 katika miradi yote zimekwishatolewa.

ii. kusaidia ukuaji wa Uchumi wa maeneo hayo kwa kuimarisha hali ya usafiri, Ukuaji wa Sector binafsi katika biashara, Uimarishaji wa sekta ya Afya na Upatikanaji wa Chakula kwa ujumla katika maeneo yote yanayozunguka mradi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *