SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI POLEPOLE NCHINI MALAWI

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole baada ya kuwasili leo Julai 10, 2022 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini humo.

Mhe. Spika atashiriki Mkutano wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) utakaoanza tarehe 11 hadi 16 Julai, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Bingu (BICC) Jijini Lilongwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *