
Mbunge wa jimbo la Ukonga amefanya ziara katika kituo cha afya Majohe kuona maendeleo ya ujenzi ambapo amesema kituo hicho kitasaidia kuwaondolea adha wananchi wa maeneo hayo ambapo walikuwa wanatembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu hasa kwa mama wajawazoto na huduma za upasuaji.
Aidha Silaa ameipongeza swrikali ya Rais Samia kwa kuwajali wananchi wake.
Kwa upande wake Mganaga Mfawidhi Zahanati ya Majohe Rosemary Amlima amemshukuru Rais Samia kwa kuwaletea kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi huo ambapo amesema ujenzi huo ukikamilika utasidia wakazi hao kwani madaktari bingwa pamoja na wodi ya wazazi itakiwepo masaa 24.

Diwani wa kata ya Majohe Mohamedi Ngonde amesema wakazi wa maeneo hayo walikuwa wanapata adha kubwa wanaenda kufuata huduma Pugu,Chanika na Kisarawe ambapo ilisababisha mama wajawazito kufariki kwa kukosa huduma.
