MTATIRO AAPISHWA KUWA WAKILI

Katika sherehe za 66 za kupokea Mawakili wapya leo, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Julius S. Mtatiro Esq. ni miongoni mwa mawakili wapya 335 walioapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma kuwa Mawakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama zilizopo chini yake isipokuwa Mahakama za Mwanzo.

DC Mtatiro ana shahada za juu takribani nne, ambazo ni Shahada ya Sanaa katika elimu (BAED), Shahada ya Sheria (LLB), Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Umma (MPA), Shahada ya Uzamili ya Sera za Umma (MAPP), Stashahada ya Juu ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo (PDLP), Cheti cha Juu cha Uongozi na Cheti cha Juu cha Tafsiri na Ukalimani kati ya Lugha ya Kiingereza na Kiswahili na vyeti vingine vingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *