Waganga wakuu wa mikoa na wilaya endeleeni kutoa elimu ya kujikinga na Uviko-19- Bashungwa

OR TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Miitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuendelea kuelimisha watanzania umuhimu wa chanjo ya Uviko-19.

Bashungwa ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha pamoja kati ya Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Dkt. Ted Chaiban, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye ni mratibu mkuu wa kitaifa wa mapambano dhidi ya UVIKO – 19.

Kikao hicho kimelenga kujadili namna ya kuendeleza mapambano ya ugojwa wa UVIKO-19.

Amesema utoaji wa chanjo ya Uviko-19 ni hiyari na kuwa ni vyema wakahakikisha wanatoa elimu ya faida ya chanjo hiyo na kuwa isiwe kikwazo cha utoaji wa huduma kwa jamii wakiwemo wajawazito.

Bashungwa amaeelekeza mkazo mkubwa uelekezwe kwenye utoaji wa elimu kwa umma juu ya faida za chanjo na sio kutumia kigezo cha kuwalazimisha kupewa chanjo ndio wapatiwe huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya.

” Chanjo ya UVIKO-19 ni muhimu lakini ni suala la hiyari ya mtu, hivyo mhakikishe manaelimisha wananchi umuhimu na faida za chanjo na sio kulazimisha kuchanja ndio apatiwe huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya.”

“Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya tukisikia kuna Mama mjawazito aliyeenda kupata huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya, akalazimishwa apawe chanjo ya UVIKO 19 kuwa ndio kigezo cha kupatiwa huduma huyo tutamchukulia hatua za kinidhamu.”

Bashungwa amewataka Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kutekeleza waji wao wa kusimamia ipasavyo vituo vya kutolea huduma za afya nchi nzima ili kutolewa huduma bora kwa wananchi.

Aidha, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasssan mwongozo na dira nzuri ya kuelekeza fedha za mapamabo ya UVIKO 19 kwa kujenga miundombinu katika sekta ya afya kununua vifaa tiba vilevile sekta ya elimu kujenga madarasa zaidi ya 15,000.

Kwa Upande wake, Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu ameeleza kuwa haja ya wataalamu wa afya na jamii ya Watanzania kuendelea kutekeleza afua za kupambana na UVIKO 19 ikiwamo kupata chanjo.

Amesema tishio la ugonjwa huo bado lipo na kuitaka jamii kufuata ushauri wa walaamu wa afya ili kujikinga na kuzuia kuenea kwa uognjwa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *