NCHIMBI ACHUKUA FOMU, KUGOMBEA UWENYIKITI UVCCM TAIFA

Mratibu wa miradi katika kampuni Tanzu ya chama Cha Mapinduzi, Jitegee Trading Company Limited, Ndugu Vianelly Vian Nchimbi amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya Uwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)

Nchimbi amechukua fomu hiyo katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya Umoja huo zilizopo Upanga Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kuchukua fomu Nchimbi alipata fursa ya kuzungumza na Vyombo vya Habari na kueleza moja ya Vipaumbele vyake ni kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita kujenga Uchumi imara wa vijana bila kujali itikadi zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *