CHIFU KUTOKA CAMEROON AVUTIWA NA BUSTANI YA WANYAMAPORI

Chifu Fuanken Achankeng kutoka Cameroon ameeleza kuvutiwa na Wanyama waliopo ndani ya bustani ya Wanyamapori hai iliyopo ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii Katika Maonesho ya 46 ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Akiwa ameambatana na mkewe pamoja na ujumbe wa maprofesa kutoka Cameroon Chifu Fuanken amesema amefurahishwa sana na Wanyama aliowaona katika bustani ya Wanyamapori hiyo na kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa juhudi za kuhifadhi Wanyamapori hapa Nchini.

“Tanzania ni Nchi iliyobarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za Wanyamapori na vivutio vya kipekee Duniani” amesema

“Naipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa jitihada za kuhifadhi na kulinda rasilimali Wanyamapori hapa Nchini” ameongeza

Aidha maofisa wa TAWA wametumia fursa hiyo kuuelezea ugeni huo tabia za Wanyamapori hao na mchango wao katika kukuza pato la Taifa kupitia sekta ya Utalii Nchini kitendo ambacho kiliwafurahisha wageni hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *