
Na Mwandishi Wetu
Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma umeendelea kukamilishwa kujengwa kwa kasi huku hatua ya sasa ikiwa inaelekea kwenye kufanya ukamilisho utakozifanya Wizara hizo ziwe za kisasa na zenye mvuto unaoendana na maelekezo ya Serikali.
Hayo yamesemwa leo (tarehe 5/7/2022) leo na Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Mratibu wa ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma Bw Meshach Bandawe wakati akiongoza kikao cha mkakati wa kukamilisha ujenzi wa ofisi za Wizara zinazojengwa awamu ya pili katika Mji wa Serikali ambacho yeye akiwa Mwenyekiti.
Amesema kwa hatua ambazo miradi hiyo inakwenda sasa kuna umuhimu wa kukaa na wataalamu wanaotekeleza ukamilishaji wa Wizara hizo ili kuwa na ukamilishaji wenye mvuto na utakaofanya majengo hayo yawe ya kisasa zaidi ikizingatiwa kuwa miundombinu iliyojengwa na inayoendelea kujengwa kama vile barabara za lami, uwekaji taa za barabarani, majengo ya kisasa na miundombinu mingine imefanya mji huu kuwa na mvuto wa kipekee kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Amesema madhari iliyopo inaendelea kuratibiwa kwa umahiri wa hali ya juu kwa kuzingatia miongozo iliyowekwa na ushirikishwaji wa Makatibu Wakuu husika,
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Kyando Mchechu ambaye aliongoza timu ya Wataalamu kutoka kwa Waendelezaji na Wajenzi alisema Shirika la Nyumba na Wadau wengne wanahakikisha wanafanya ukamilishaji wa kisasa na unaozingatia mahitaji yote muhimu yalioainishwa na miongozo.

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Mratibu wa ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma Bw Meshach Bandawe akiongoza kikao cha mkakati wa kukamilisha ujenzi wa ofisi za Wizara zinazojengwa awamu ya pili katika Mji wa Serikali.

Sehemu ya wataalamu wa ujenzi na Washauri pamoja na wajengi wakifuatilia kikao cha mkakati wa kukamilisha ujenzi wa ofisi za Wizara zinazojengwa awamu ya pili katika Mji wa Serikali. Kilichofanyika leo mchana Jijini Dodoma.
