WADAU WAUNGA MKONO MPANGO WA UENDELEZAJI JIJI LA DODOMA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemiah Kyando Mchechu amewasilisha kwa wateja wa nyumba za makazi za NHC Medeli, Dodoma wengi wao wakiwa Wabunge, Mpango wa Uendelezaji Jiji la Dodoma unaoanza kutekelezwa na NHC.
Katika wasilisho lake, Bw. Mchechu Shirika la Nyumba la Taifa limefanya upendeleo wa makusudi kwa Jiji la Dodoma likiwa ni la pili kutoka Jiji la Dar es Salam lengo likiwa ni kuunga mkono lengo la Serikali kuhamia Dodoma kwa kuwapatia wakazi wa jiji hilo nyumba bora.
Mchechu ameyasema hayo jana katika wasilisho lake kwa wateja hao kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkandarasi House Jijini Dodoma jana (Juni 30, 2022) jioni.
Katika maelezo yake kwa wateja hao ambao wamekongwa vilivyo na mikakati ya Shirika, Mkurugenzi Mkuu ameeleza kuwa Shirika litaanza baadaye mwezi huu ujenzi wa nyumba za makazi katika maeneo ya Medeli II, Njedengwa na Katikati ya Jiji ambako kutajengwa maeneo ya maduka makubwa.
Nyumba zote za Medeli zipatazo 190 zilijengwa kwa ajili ya kuuzwa, lakini kutokana hali ya uchumi ya wakati ule nyumba 50 zilipangishwa na sasa zinauzwa kwa wateja wanaoishi ndani ya nyumba hizo ili fedha itakayopatikana itawekezwa kwa ajili ya kuendeleza miradi mingine ya Dodoma na maeneo mengine.

Akizungumza baada ya kuwasilishwa kwa Mpango huo, Mweka Hazina wa Chama cha Wenye Nyumba NHC Medeli, Omari Kigua ambaye pia ni Mbunge wa Kilindi amempongeza Bw. Mchechu kwa kuaminiwa tena na Mheshimiwa Rais na akaipongeza mikakati yake mikubwa ya ujenzi wa nyumba ambazo zitawanufaisha Watanzania wengi.
Amesema miongoni mwa makazi bora kabisa yaliyopo Jijini Dodoma ni NHC Medeli na akasema wakazi wa nyumba hizo wamekuwa wakiishi Maisha mazuri na akashauri zijengwa nyumba nyingi Zaidi katika maeneo mengine Dodoma ili kuboresha makazi bora Dodoma.
Naye Mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe. Philipo Mulugo amepongeza hatua hiyo na akasema wao kama wadau wanahitaji kuwa mpango mzuri wa kupata fedha za kukopa ili aweze kufaidika na matunda ya mradi huo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na baadhi ya mabenki wakiwamo NMB, CRDB, First Housing Finance na Azania Bank waliowasilisha kwa wateja hao aina ya mikopo wanayotoa na namna wabunge na wateja hao watakavyofaidika. Takribani wateja wote wanaopanga wamejaza fomu za kununua nyumba hizo kwa ajili ya kuzinunua.

Picha zifuatazo zinaonyesha tukio hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkandarasi House Jijini Dodoma jana (Juni 30, 2022).

Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemiah Mchechu akiwasilisha mada ya Mpango wa Uendelezaji Jiji la Dodoma unaoanza kutekelezwa na NHC.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Mchechu akiwa pamoja na baadhi ya wateja hao kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkandarasi House Jijini Dodoma jana (Juni 30, 2022) jioni wakati Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa NHC, William Genya (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Mchechu akiwa pamoja na baadhi ya wateja hao kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkandarasi House Jijini Dodoma jana (Juni 30, 2022) jioni wakati Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa NHC, William Genya (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *