PROF. SHEMDOE AKAGUA MAANDALIZI YA UMISSETA&UMITASHUMTA 2022

OR-TAMISEMI, TABORA

Katibu Mkuu OR- TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe ametembelea Shule ya Wavulana ya Tabora na Shule ya Wasichana Tabora kukagua viwanja vya michezo vitakavyotumika katika Mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA kwa mwaka 2022.

Katika ukaguzi huo uliofanyika Tarehe 28.06.2022 Prof Shemdoe ameelekeza Kamati ya Maandalizi ya Michezo hiyo kuhakikisha masuala muhimu yote yanakamilika kabla ya kuanza Mashindano hayo kuanza.

‘Nahitaji kuona maandalizi ya viwanja vyote vitakavyotumika katika mashindano hayo pamoja shule zitakazotika kwa ajili malazi kukamilika mapeema kusubiria siku ha ufunguzi wa mashindano hayo’ amesisitiza Shemdoe.

Idadi ya Wanafunzi wanaotarajiwa kushirikia mashindano hayo kwa Mwaka huu wa 2022 ni 3600 kwa upande wa UMISETA na 3320 kwa upande wa UMITASHUMTA Tanzania Bara na Visiwani.

Hakikisheni maandalizi ya viwanja na malazi yote yakamilike hataka ili watoto watakapofika wafirahie kushirikiki katika mashindano hayo makubwa yanayolenga kukuza vipaji wa watoto kimichezo.

Katika hatua nyingine baadhi ya walimu wa shule za Mkoa wa Tanora wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha maslahi ya Watumishi na mazingira ya kujifunza na kufundishia.

Mashindano ya UMITASHUMTA yatafanyika kuanzia Tarehe 29/07 – 09/08 na UMISSETA yataunguruma kuanzia Tarehe 09 -19/08/2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *