SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA WASANII WA WCB

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii wa WCB akiwemo Zuchu, Mbosso, Lavalava pamoja na Viongozi kutoka Wasafi Media akiwemo Spencer Lameck na Dorice Mziray walipokutana katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo Juni 29, 2022 Wakati Mhe. Spika akielekea Dar es salaam kushiriki Kongamano maalum la Viongozi wa dini la kuhamasisha Sensa ya watu na makazi.

Wasanii hao pia wanatarajiwa kushiriki hafla maalum na Waheshimiwa Wabunge itakayofanyika katika Viwanja vya Bunge leo hii Jijini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *