MWANASHERIA MKUU AHIMIZA UWEPO WA JUKWAA LA WAENDELEZAJI MILIKI

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dk. Eliezer Feleshi, ametaka kuwepo kwa jukwaa la pamoja la wadau wa uendelezaji miliki ili kusudi kuweza kuvuna faida za kushirikishana fursa na changamoto zitakazoiwezesha sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa nchi kukuwa kwa haraka na kulisaidia Taifa.

Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Kyando Mchechu na Menejimenti yake pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) jijini Dodoma leo (tarehe 28/6/2022), Mhe. Jaji Dk. Eliezer Feleshi amesema Ofisi yake iko tayari kuweka na kujenga mazingira bora ya kisheria yatakayoiwezesha sekta hiyo ikakua na hatimaye kukuza uchumi wa Taifa.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dk. Eliezer Feleshi akiwa katika kikao cha pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Kyando Mchechu na Menejimenti yake pamoja na watendaji wa TBA.

“Nimekubali wito wenu kuja kunishirikisha kuhusu umuhimu wa jambo hili kwa mustakabali bora wa nchi maana nimeona mambo makubwa mnayafanya, lakini mkiwa kila mmoja na lake nahamna formal forum ya real estate ninafikiri hicho kitu kinatakiwa kiwepo na uwapo wake utawawekea mazingira bora na Ofisi yangu iko wazi kwa hili changamkieni fursa,”amesema.

Amesema kuwa angependa awape urahisi wadau hao katika ufanisi wa kazi kwani taasisi hizo za umma zinafanya majukumu tofauti yenye lengo moja la kustawisha sekta ya makazi, hivyo hakuna budi kuwajengea mazingira bora.

Jaji Feleshi alizitaja baadhi ya taasisi hizo zinazoshughulika na uendelezaji miliki kuwa ni pamoja na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Watumishi Housing Investment na kusema zote hizo zina fursa ya kufanya vizuri zaidi zikijengewa mazingira ya kisheria na kiufanisi.

Amesema anatambua changamoto ya ukusanyaji wa madeni yanayozipata taasisi hizo wadaiwa wakubwa wakiwa ni Serikali, hivyo angependa apate taarifa na mikakati iliyopo ili ajue aweze kurahisisha mazingira ya kisheria yatakayoweza kuwafanya wanaodaiwa kuwajibika kisheria.

Ametoa muda wa wiki mbili kuanzia sasa ili awasilishiwe ripoti ya madeni ikiwa na vikwazo wanavyokabiliana navyo ili kuweza kutoa muongozo mzuri utakaoongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Kyando Mchechu amechukua fursa hiyo kumshukuru Mwanasheria Mkuu wa hatua yake hiyo muhimu inakuja kuifungua sekta ya ujenzi na hivyo kusaidia makuzi ya nchi.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dk. Eliezer Feleshi akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Kyando Mchechu na Menejimenti yake pamoja na watendaji wa TBA.

“Kwa niaba ya wadau wenzangu nikushukuru kwa hatua hii kwa ni hatua muhimu sana kwa nchi yetu, tukiunda jukwaa la ushirikiano ni bora kwasababu
hatushindani, lakini tunasaidiana kukidhi mahitaji ya Watanzania, mahitaji ni makubwa na sisi peke yetu hatuwezi kukidhi kiu ya soko isipokuwa tukiwa wamoja tutafika mahali pazuri,”amesema Mchechu.

Amesema sekta ya uendelezaji miliki ni uchumi mkubwa sana na inaajiri watu wengi hawa watu wanahitaji kuwa jukwaa lao la kuzungumza mambo yao na uwapo wa fursa nzuri kama hizo ni jambo jema ameahidi kuwasilisha ripoti inayotakiwa na Mwanasheria Mkuu mapema wiki ijayo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dk. Eliezer Feleshi akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Kyando Mchechu mara baada ya kufanya kikao na NHC na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) leo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dk. Eliezer Feleshi akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Kyando Mchechu na Menejimenti yake pamoja na watendaji wa TBA.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dk. Eliezer Feleshi akiwa katika kikao cha pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Kyando Mchechu na Menejimenti yake pamoja na watendaji wa TBA.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dk. Eliezer Feleshi akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Kyando Mchechu mara baada ya kufanya kikao na NHC na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *