DKT.MAGEMBE AWASHUKURU WANANCHI UTEKELEZAJI WA MIRADI

Naibu Katibu Mkuu Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Grace Magembe amewashukuru wananchi kwa kuwa wazalendo kwa kuchangia nguvu kazi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini .

Amewataka kuendeleza ari hiyo kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo nchini, akisisitiza kuwa ushirikishwaji wa wananchi katika utekelezaji wa miradi unapunguza gharama za ujenzi,unatoa ajira kwa vijana , unaimarisha usimamizi , ulinzi na kuwafanya wananchi wamiliki wa miradi hii.

Hayo yamebainishwa tarehe 27 Juni 2022 katika ziara ya Dkt. Magembe alipokuwa anakagua ujenzi wa miundombinu pamoja utoaji wa huduma katika Kituo cha afya Rubare kilichopo Halmashauri ya Wilaya Bukoba Mkoani Kagera.

“Kupitia kituo hiki cha Rubare nitoe shukrani kwa wananchi wote ambao wameshirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Serikali inathamini mchango wa nguvu kazi,usimamizi kupitia kamati mbalimbali mlizounda,utoaji wa maeneo ya ujenzi na mengineyo mmethibitisha kuwa maenedeo yetu watanzania yanaletwa na sisi wenyewe” Dkt. Magembe

Aidha Dkt. Magembe hakuridhishwa na utekelezaji wa ujenzi Kituo cha Afya Kashai kilichopo Manispaa ya Bukoba ambacho kipo nyuma ya utekelezeaji kwa miezi 6, amemuelekeza Mkurugenzi kuwasilisha maelezo ya kilichopelekea ucheleweshwaji huo sambamba na mpango kazi wa ukamilishaji wa mradi huo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -TAMISEMI ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *