WAZIRI BASHUNGWA APOKEA KITABU CHA UFAHAMU MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA MAJIMBO YA UCHAGUZI TANZANIA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amekutana na kufanya mazungumzo na Ndugu Fidelis Ndahama Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamii Business na mwandishi wa kitabu cha Ufahamu Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Majimbo ya Uchaguzi Tanzania, leo juni27, 2022 jijini Dodoma.

Ndugu Fidelis Ndahama amepata fursa ya kutambulisha kitabu chake cha Ufahamu Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Majimbo ya Uchaguzi Tanzania kilichochambua kwa undani sheria ya mfuko wa Jimbo na mfumo wa uibuaji miradi ya maendeleo ya jimbo.

Kitabu hicho kinajenga uelewa wa matakwa ya sheria ya mfuko wa jimbo ambao utaimarisha dhana ya uwajibikaji na utekelezaji wa sheria ya mfuko wa jimbo ili kuchochea maendeleo ya wananchi kupitia miradi yao pendekezwa ambayo haifadhiliwi na Bajeti kuu ya Serikali kila mwaka wa fedha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *