TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA MPYA ZA UALIMU NA KADA ZA AFYA

1. UTANGULIZI

Ndugu Wanahabari;

Mtakumbuka kuwa mwezi Aprili, 2022; Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alitoa kibali cha ajira kwa kada za Ualimu na Afya, kwa ajili ya kuajiri walimu 9,800 wa Shule za Msingi na Sekondari, na wataalam wa Afya 7,612.

Baada ya kupata kibali cha ajira, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ilitoa tangazo kwa wahitimu mbalimbali wa Ualimu na Kada za Afya, kuwasilisha maombi ya kazi, kupitia mfumo wa kielektroniki wa kupokea na kuchakata maombi ya ajira, kuanzia tarehe 20/04/2022 hadi 08/05/2022. Jumla ya maombi 165,948 yakiwemo ya Wanawake 70,780 na Wanaume 95,168 yaliyopokelewa kwenye mfumo, ambapo maombi ya Kada za Afya ni 42,558, na Kada ya Ualimu ni 123,390.

Ndugu Wanahabari;

Ili kufanikisha mchakato wa ajira, Ofisi ya Rais – TAMISEMI iliunda Timu Maalum, ya kufanya Uchambuzi wa Maombi ya Ajira, iliyohusisha Taasisi mbalimbali. Taasisi hizo ni pamoja na Ofisi ya Rais Ikulu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania

(TCU), Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi (NACTVET), Sekretarieti ya

Ajira,    Taasisi    ya    Kuzuia    na    Kupambana    na      Rushwa

(TAKUKURU), na Mabaraza ya Kitaalamu katika Sekta ya Afya.

(a) Vigezo Vilivyotumika

Ndugu Wanahabari;

Kutokana na idadi ya waombaji kuwa kubwa, Timu ya Uchambuzi wa Maombi ya Ajira ilipewa vigezo vilivyoandaliwa kama mwongozo wa kutoa ajira kwa waombaji, kwa lengo la kuhakikisha uwepo wa haki na uwazi katika zoezi hili. Katika kuhakikisha usawa wa kijinsia unafikiwa, katika vigezo vilivyotumika kupata waajiriwa wapya kwa mwaka 2022, kila kigezo kilizingatia uwiano wa kijinsia. Vigezo vilivyotumika ni kama ifuatavyo: –

i. Mwaka wa kuhitimu

Katika kigezo hiki, kipaumbele kimetolewa kwa waombaji wenye sifa waliotangulia kuhitimu kwa mfuatano wa mwaka, kulingana na hitaji la kada/kozi au kiwango cha Elimu, na pia mwaka wa kozi ilivyoanza kutoa wahitimu.

ii. Umri wa kuzaliwa

Waombaji wenye sifa waliopangwa kwa mujibu kigezo namba (i) hapo juu walipangwa kulingana na umri wa kuzaliwa. Lengo ni kuwawezesha waombaji wenye umri unaokaribia miaka 45 kuingia katika utumishi wa umma kwa masharti ya kudumu, kwa mujibu wa Sera ya Ajira Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma toleo la Pili la mwaka 2008.

iii. Waombaji Wenye Ulemavu

Uchambuzi wa maombi ya watu wenye Ulemavu ulifuata vigezo vyote vya mwaka wa kuhitimu na umri wa kuzaliwa, vilivyooneshwa kwenye kipengele cha (i) na (ii). Hata hivyo, vigezo hivi vilitumika kuwashindanisha waombaji wenye ulemavu peke yao, kwa kuzingatia takwa la Sheria ya Watu Wenye Ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010, kifungu cha 31 (1)-(3). Uchambuzi huu ulifanywa kwa ushirikiano na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu. 

Ndugu Wanahabari

Mchakato wa uchambuzi wa maombi ya ajira ya Kada za Afya na

Ualimu ulizingatia utaratibu ufuatao:-

  1. Kwanza, ilihusisha uchambuzi wa moja kwa moja kutoka kwenye mfumo wa maombi. Mfumo huu umewezesha waombaji wote wenye sifa kupata ajira kwa haki na usawa, kama yalivyo maelekezo ya Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwamba Watanzania wote wenye Sifa wapate ajira bila upendeleo. Hivyo mfumo huu uliwachuja waombaji awali kwa kuzingatia mahitaji ya kibali cha ajira kilichotolewa, ukamilifu wa viambata vilivyohitajika kwa mwombaji, na mwaka wa kuhitimu waombaji; na 
  2. Pili, uchambuzi wa kina ulifanyika ukihusisha pia uhakiki wa nyaraka za maombi yaliyopata uzito wa juu, kulingana na vigezo vilivyowekwa.

2. KUHUSU UZINGATIAJI WA MAHITAJI NA MSAWAZO

SAWA WA WATUMISHI

Ndugu Wanahabari

Upangaji wa watumishi wa Kada za Afya na Ualimu katika Vituo vya kutolea huduma za Afya na shule, umezingatia mahitaji ya watumishi katika mikoa husika. Kutokana na juhudi za Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Sita, Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika kufanya maboresho makubwa ya Sekta ya Afya, upangaji wa watumishi wapya umezingatia mahitaji ya watumishi katika Halmashauri zenye Hospitali mpya, Vituo vya Afya vipya, na Zahanati mpya zilizokamilika ambazo zimeshindwa kutoa huduma za msingi, kutokana na kukosa watumishi wenye sifa, pamoja na Halmashauri zenye upungufu mkubwa wa watumishi hao. Aidha, kwa upande wa kada za Ualimu, utaratibu wa upangaji ulizingatia mgawanyo wa nafasi kwa kila somo, na kiwango cha Elimu kulingana na hitaji la kibali. 

Mchakato huu wa ajira umetoa fursa kwa waombaji kutoka mikoa yote ya Tanzania, hivyo basi upangaji wake umezingatia uzalendo na utamaduni wetu, kuwa kila mtanzania anaweza kufanya kazi mahali popote nchini.

3.  WAOMBAJI WALIOKIDHI VIGEZO NA KUPANGIWA VITUO (a) Waombaji wa Kada za Afya Ndugu Wanahabari

Kwa upande wa kada za Afya, Waombaji wenye sifa waliokidhi vigezona kupangiwa vituo vya kazi ni 6,876 wanawake ni 3,217 sawa na asilimia 46.8 na wanaume ni 3,659 sawa na asilimia 53.2 wakiwemo wenye ulemavu 42 sawa na asilimia 0.61 kutokana na uchache wa waombaji wenye sifa wa kundi hilo.

Aidha, nafasi 736 kada za Afya zilikosa waombaji wenye sifa. Kada hizo ni Daktari wa Meno (50), Tabibu Meno (43), Tabibu Msaidizi (244), Mteknolojia Mionzi (86) na Muuguzi- ngazi ya cheti (313). Kada hizi zitarudiwa kutangazwa ili kupata waombaji wenye sifa watakaojaza nafasi hizo.

Ndugu Wanahabari 

Mchanganuo wa idadi ya wataalamu wa Kada za Afya waliopata nafasi za ajira umeoneshwa kwenye Jedwali la 1.

Jedwali la 1: Mchanganuo wa Waombaji waliopata ajira wenye Ulemavu na Wasiokuwa na Ulemavu

Na.KadaWasiokuwa na ulemavuWenye UlemavuJumla
1Afisa     Afya     Mazingira      Msaidizi Daraja la II982100
2Afisa Lishe Daraja la II41142
3Afisa Muuguzi Daraja la II (NO)68270
4Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II1782180
5Afisa Ustawi wa Jamii Daraja la II381250
6Daktari Daraja la II (MD)6511652
7Fundi Sanifu Vifaa Tiba (Biomedical Engineering Technician) Daraja la II102 102
8Katibu wa Afya Daraja la II69170
9Mfamasia Daraja la II102 102
10Msaidizi       wa       Afya        (Medical Attendant)3928400
11Mteknolojia – Dawa Daraja la II250 250
12Mteknolojia – Maabara Daraja la II1973200
13Mteknolojia Msaidizi – Maabara1491150
14Muuguzi Daraja la II3,07423,076
15Tabibu Daraja la II (CO)1,26761,273
16Mteknolojia – Mionzi Daraja la II34 34
17Tabibu Meno Daraja la II69 69
18Tabibu Msaidizi55156
Jumla Kuu6,834426,876

(b) Waombaji wa Kada za Ualimu

Ndugu Wanahabari

Kwa upande wa kada za Ualimu, Waombaji wenye sifa waliokidhi vigezona kupangiwa vituo vya kazi ni 9,800 ambapo jumla ya walimu 5,000 wamepangwa shule za Msingi na walimu 4,800 Shule za sekondari, wakiwemowalimu wenye ulemavu wa shule za Msingi na Sekondari 261.

Kati yaWalimu 5,000 washule za Msingi wanawake ni 2,353 sawa na asilimia 47.06 na wanaume ni 2,647 sawa na asilimia 52.94. Kwa upande wa walimu 4,800 wa Shule za sekondari wanawake ni 1,289 sawa na asilimia 26.85 na wanaume ni 3,511 sawa na asilimia 73.15. Aidha, walimu wenye ulemavu 261 wa shule za Msingi na Sekondari walioajiliwa ni sawa na asilimia 2.66 ya walimu wote walioajiliwa wakiwemo wanawake 84 na wanaume 177. Napenda ieleweke pia kuwa, kwa walimu wa sekondari tumetoa ajira za walimu wa sayansi kwa asilimia 76 ya nafasi 4,800 tulizopewa.

Ndugu Wanahabari 

Mchanganuo wa idadi ya walimu waliopata ajira kwenye kada mbalimbali za ualimu umeoneshwa kwenye Jedwali la 2.

Jedwali 2: Idadi ya walimu waliopangwa kuzingatia nafasi zilizoainishwa katika kibali

IdaraKiwango Cha ElimuJuml a
MsingiBachelor Degree Education (Arts)74
Bachelor of Education in Early Childhood Education500
Certficate in Early Child Education15
Certificate in Primary Education2,195
Certificate in Primary Education – Physical Education2
Certificate in Primary Education – Special Education135
Diploma in Early Child Education1,000
Diploma in Primary Education1,000
Diploma in Secondary Education (Arts)79
Jumla ndogo Msingi5,000
    Sekondar iBachelor Degree Education (Science)1,768
Bachelor Degree Education (Arts)680
Bachelor Degree Education (Business)70
Diploma in Secondary Education (Arts)360
Diploma in Secondary Education (Business)16
Diploma in Secondary Education (Science)1,901
Diploma in Secondary Education- Physical Education5
Jumla ndogo Sekondari4,800
Jumla Kuu9,800

4. SHUKRANI KWA MHE. RAIS

Ndugu wanahabari

Tunamshukuru sana Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea kutekeleza sera ya elimu bila ada, ambapo pamoja na mambo mengine, imepelekea watoto ambao walikuwa hawawezi kusoma kutokana na kushindwa kulipiwa ada, kwenda mashuleni. Kutokana na ongezeko la wanafunzi kupitia sera hii, uhitaji wa walimu na miundombinu ya madarasa umeongezeka. Katika kukabiliana na changamoto hii, kwa kipindi cha miezi 15 aliyokuwepo madarakani, Rais wetu mpendwa ametuwezesha kujenga madarasa 15,000 kupitia fedha za mkopo wa IMF, na kutupatia kibali cha kuajiri watumishi wa elimu 9,800 na wa afya 7612. Aidha, katika mwaka 2020/21 Serikali iliajiri watumishi 23,000 kada ya elimu na afya. Hatua hizi zinazochukuliwa na Mhe.

Rais zinastahili kupongezwa sana.

5. MAELEKEZO YA WAZIRI

Ndugu wanahabari

Napenda kutumia fursa hii kutoa maelekezo ya Msingi mbalimbali yanayopaswa kuzingatiwa na Waajiriwa na Waajiri.

  1. Waajiriwa wapya wote wahakikishe wanaripoti kwa Wakurugenzi wa Halmashauri walizopangiwa wakiwa na Kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho ya NIDA, Cheti halisi cha kuzaliwa, Vyeti Halisi vyote vya Taaluma na Utaalamu wa Kazi vya mwajiriwa, ili vihakikiwe na Mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira;
  • Waajiri wote wahakikishe wanapokea vyeti na kuviwasilisha baraza la mitihani kwa ajili ya uhakiki. Wizara ipewe taarifa mara moja kwa wale watakaokutwa na vyeti ambavyo ni vya kugushi ili hatua kali zichukuliwe;
  • Waajiri wote wahakikishe watumishi wapya waliopangwa kwenye Halmashauri, wanapewa barua za ajira, na kuripoti kwenye vituo

walivyopangiwa tu, na si vinginevyo;

  • Mwajiriwa mpya atakayechukua posho ya kujikimu, na baadaye asiripoti katika kituo chake cha kazi alichopangiwa, atachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria;
  • Waajiriwa wapya ambao hawataripoti katika vituo walivyopangiwa ndani ya siku 14, kuanzia tarehe ya tangazo hili, watakuwa wamepoteza nafasi zao ambazo zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa, waliopo kwenye Kanzidata (Database) ya Ofisi ya

Rais – TAMISEMI;

  • Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo Waajiriwa wapya wamepangwa, wahakikishe wanawapokea Waajiriwa wapya na kuwawezesha kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma, na baadaye kutoa taarifa ya kuripoti kwao. Taarifa za kuripoti waajiriwa hao zijazwe kwenye mfumo wa kielektroniki (ajira.tamisemi.go.tz), baada ya kila mtumishi kupokelewa na kukamilisha taratibu;
  • Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaelekezwa kukamilisha taratibu za ajira haraka, ili waajiriwa wapya waingizwe kwenye mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara

(HCMIS) mapema iwezekanavyo;

  • Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wote wa Halmashauri, kuhakikisha wanatekeleza maagizo ya OR-TAMISEMI yaliyotolewa kwenu Mwezi Machi, 2022, ya kuhakikisha mnafanya msawazo wa IKAMA ya walimu wa Shule za Msingi na Sekondari, ndani ya Mkoa na Halmasgauri kabla au ifikapo tarehe 30 Juni, 2022. Tekelezeni kwa biddi maelekezo hayo ili kuhakikisha shule zinakuwa na uwiano mzuri wa walimu, na taarifa ya utekelezaji iwasilishwe kabla au ifikapo tarehe

15 Julai, 2022. OR-TAMISEMI haitasita kumchukulia hatua Mwajiri ambaye hatatekeleza maelekezo haya ya kufanya msawazo wa walimu katika kuleta uwiano wa mwalimu, na wanafunzi wa 1:60 ulioelekezwa; 

  1. Tunawaelekeza Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu kushirikiana na Bodi zao za shule ili kufuata miongiozo ambayo Wizara imetoa kwa ajili ya michango ya wanafunzi wanaoendelea na masomo. Hatua kali zitachukuliwa kwa Mkuu wa Shule au Mwalimu Mkuu yeyote ambaye ataenda kuinyume na miongozo iliyotolewa na Serikali; na
  • Walimu waliopo kazini na Waajiriwa wapya, kuhakikisha wanafundisha wanafunzi kwa weledi, na bidii ya hali ya juu kwa kuzingatia kalenda ya ufundishaji iliyopo. Wakuu wa Shule, Waratibu Elimu Kata, Maafisa Elimu wa Halmashauri na Mikoa yote nchini kufuatilia ufundishaji wa kila siku darasani, na kujiridhisha kuwa wanafunzi wanapata umahiri unaotarajiwa kwenye ngazi mbalimbali za elimu ya Msingi na Sekondari. Aidha, Watumishi wote wa kada za Afya nchini, wanaoendelea na utumishi, na walioajiriwa wapya, kuhakikisha wanawahudumia wananchi kwa weledi na upendo wa hali ya juu, kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo ya utoaji bora wa huduma za afya nchini.

Ndugu Wanahabari

Majina ya waombaji wote waliopangiwa vituo vya kazi yanapatikana katika Tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI www.tamisemi.go.tz.

Asanteni kwa kunisikiliza.

Innocent L. Bashungwa (Mb.)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *