SPIKA DKT. TULIA ALIONGOZA BUNGE KUFANYA MAANGAMIZI CRDB

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson Leo Juni 25, 2022 Jijini Dodoma amewaongoza Wabunge katika Bonanza la CRDB PAMOJA na kufanikiwa kubeba Vikombe pamoja na Medali

Katika Mashindano mbalimbali Timu za Bunge zimefanikiwa kuibuka Vinara

Spika Dkt Tulia Ackson amechukua Medali baada ya kuibuka mshindi katika Mbio fupi za Mita 100

Kwa Upande wa Mpira wa Miguu Timu ya Bunge imeshinda Kikombe na kupata Medali baada ya kufanya vyema katika Michezo yao.

Pia Timu ya Bunge kwa Upande wa Mpira wa Pete ikiongozwa na Timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar nayo imefanikiwa kubeba Kikombe sambamba na Medali baada ya kuifunga CRDB 9-7

Bonanza la CRDB PAMOJA limeanza mapema alfajiri kwa Matembezi(Jogging) kuanzia katika Viwanja vya Bunge hadi uwanja wa Jamhuri na baadae kufuata michezo mbalimbali ikiwemo kuruka kamba, mchezo wa Bao, Mbio, Mpira wa Miguu, pamoja na Mpira wa Pete

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *