
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), ameibuka mshindi kwenye mbio za mita 100 zilizoshirikisha Viongozi Wanawake wakati wa tamasha la *CRDB Bank Pamoja Bonanza* katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma leo Juni 25, 2022.Katika mbio hizo walishiriki Mawaziri, Naibu Mawaziri, Wabunge na viongozi kutoka benki ya CRDB.
