TAMASHA LA CHOMA DAY LAITIKISA DODOMA

Usiku wa Juni 24, 2022 limefanyika Tamasha la Choma Day maeneo ya Royal Village Hotel ambalo ni kwa ajili ya Kuchoma nyama na kufurahia Burudani kutoka kwa Wasanii mbalimbali

Wasanii Waliojitokeza kutumbuiza ni pamoja na Christian Bella, Belle 9 na Bushoke.

Pia wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Kisiasa na Wabunge ambapo Mgeni Rasmi akiwa ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul.

Wakati huo huo wenyeji wakiwa ni Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa DODOMA Mjini Mhe. Antony Mavunde, Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa DODOMA Mhe. Antony Mtaka.

MATUKIO KATIKA PICHA

Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde akiwatambulisha Viongozi na Wabunge mbalimbali Waliojitokeza

Mwanamziki Christian Bella akitumbuiza katika Tamasha la Choma Day

Ikumbukwe kuwa Tamasha hilo la Choma Day hufanyika mara Moja kwa MWAKA Jijini Dodoma chini ya Ndg. Boss Ngasa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *