
Ujumbe wa TANZANIA kwenye Mkutano wa 75 la Baraza Tendaji (Executive Council) la Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) unafanyika Geneva – Uswizi, kuanzia tarehe 20 – 24/06/2022. Ujumbe wa TANZANIA unaongozwa na Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), pamoja naye ni Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji – Wizara ya Maji.
Mkutano huo, pamoja na mambo mengine, unajadili changamoto mbali mbali zinazoikabili dunia kwa sasa na namna ya kukabiliana nazo ikiwemo mabadiliko ya Tabia Nchi na namna ya kutayarisha mifumo ya kutabiliri Hali ya Hewa na wingi/upungufu wa maji (early warning systems) kwa usahihi zaidi ili kupunguza athari mbaya za kijamii na kiuchumi zinazotokana na hali mbaya ya hewa na wingi au upungufu wa maji katika maeneo mbalimbali duniani.