SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA, ELIMU NA AFYA – MSOMERA HANDENI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali imetenga na kupeleka shilingi miliomi 503.4 kufanya matengenezo ya barabara Kwenjugo – Mbagwi – Msomera yenye kilometa 32.6 ambayo ni barabara kuu kutoka makao makuu ya Wilaya ya Handeni hadi eneo la Msomera wanapohamia wakazi kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ili barabara ziweze kupitiaka wakati wote bila shida.

Pia, Serikali imetenga Milioni 716 kwa ajili ya matengenezo ya barabara za mizunguko ndani ya eneo la Msomera yenye kilomita 50 ambapo zitafunguliwa barabara mpya, matengenezo, kujengwa vivuko na kalavati ili kurahisha huduma ya kuingia na kutoka kwa Wananchi inayoenda sambamba na utengenezaji wa barabara inayounganisha kijiji cha Msomera na wilaya ya Korogwe yenye urefu wa kilomita 22.8

Ameeleza hayo Juni 22, 2022 katika mdahalo maalum wa kujadili maendeleo ya zoezi la uhamaji wa hiari kwa wakazi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kuhamia eneo la Msomera uliofanyika kwa njia ya mtandao wa Zoom na kueleza kuwa Serikali imetenga fedha nyingine katika bajeti 2022/23 shilingi bilioni 2.53 kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara wilaya ya Handeni.

Bashungwa amesema tayali ujenzi wa shule ya msingi mpya umekamilika na shule ya Sekondari mpya ambayo vyumba 7 vya madarasa vimekamilika, ujenzi wa bweni unaendelea kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji wa kukaa shuleni, ujenzi vyoo vipya vya kutosha na Ofisi za Walimu na Mahabara kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi.

Aidha, Ameeleza inakadiriwa jumla ya wanafunzi 765 watahamia eneo la Msomera ambapo wanafunzi 415 wa awali na msingi na wanafunzi 350 wa sekondari hivyo idadi ya wanafunzi hao itakuwa sambaba na kupeleka walimu katika shule hizo.

Vile vile, Bashungwa amesema tayari Serikali imetoa shilingi Milioni 500 kuanza ujenzi wa kituo cha afya kipya na shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kupanua na kuboresha huduma za afya katika zahanati ya Kijiji cha Msomera na kujenga jengo la wazazi, kuongeza watumishi na wataalam wapya katika sekta ya afya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amewataka watumishi wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma kwa kuwa Wizara hiyo imabeba taswira ya nchi.

Waziri Bashungwa amesema hayo Juni 21, 2022 kwenye Kikao kazi na Watumishi wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambapo kila mwaka huadhimishwa kuanzia tarehe 16-23 Juni.

Amewataka watumishi hao kuhakikisha wanatunza siri za Serikali na kufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma kwa kuwa TAMISEMI imebeba maisha ya watanzania.

Waziri Bashungwa ameendelea kwa kuwataka watumishi hao pia kufanyakazi kwa weledi na kujitoa katika kuwahudumia wananchi na kutojihusisha na rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

“TAMISEMI tuna jukumu kubwa la kutoa huduma kwa wananchi niwatake watumishi suala la utoaji wa huduma ni ibada tusimamie katika utendaji wa haki pasina kujihusisha na rushwa Wizara hii ni kubwa ujue ukiwa humu unatakiwa ufuate maadili ya utumishi wa Umma na imani tuwe nayo sababu sisi tunatoa huduma moja kwa moja kwa wananchi wetu” amesema Waziri Bashungwa

Amesema kuwa baadhi ya vitendo vinatokea ambavyo ni kinyume na maadili ya utumishi wa Umma ambapo baadhi ya watu wanaharibu taswira na picha ya Ofisi hii kwa kushiriki kwenye vitendo ikiwemo kugushi barua za uhamisho wa watumishi hivyo, amemuelekeza Katibu Mkuu Prof. Riziki Shemdoe kulishughulikia kwa haraka suala hilo.

“Ninaelekeza wale wote ambao waliopata barua za uhamisho ambazo tumeshafanya uchunguzi na sio halali warudishwe kwenye vituo vyao vya awali na kama kuna stahiki zozote walipatiwa ambapo ni fedha za Serikali zirudishwa na wachukuliwe hatua” amesisitiza Waziri Bashungwa

Kwa upande wa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde amewashukuru watumishi hao kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi hao kuweza kutekeleza majukumu yao ikiwa wao ni moja kwa moja wanawajibika na wananchi amewataka kuendelea kuwahudumia wananchi kwani wana imani na Wizara hiyo.

“Imani ya wananchi ni pamoja na kuwa na imani ya Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan na sisi TAMISEMI tunawajibika moja kwa moja kwa wananchi nitoe rai kwa watumishi wote kufanyakazi kwa weledi kwa kuwa tumeaminiwa hivyo tuaminike” amesema Mhe. Silinde

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe amemuhakikishia Mhe. Waziri kuwa, maelekezo yote aliyoyatoa anaenda kuyasimamia ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma amesema wao kama watendaji watahakikisha wanaendelea kushirikiana na viongozi wa ngazi zote za Wizara hiyo ili kuendelea kuwahudumia wananchi

Akiongea kwa niaba ya watumishi Bi. Namsifu Maduhu(Afisa Utumishi Mkuu) ameushukuru uongozi na kuahidi kutekeleza yale yote yaliyoagizwa kwa lengo la kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *