WATUMISHI NEC WACHANGIA DAMU, WAFANYA USAFI HOSPITALI YA UHURU DODOMA

Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma nchini ambayo kila mwaka hufanyika kuanzia tarehe 16 -23 Juni, Leo Juni 21,2022 wamejitokeza kuchangia damu na kufanya usafi katika Hospitali ya Uhuru iliyopo Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Mbali na uchangiaji Damu katika Benki ya damu ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wameshiriki kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Uhuru iliyopo Chamwino Mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma nchini ambayo kila mwaka hufanyika kuanzia tarehe 16 -23 Juni.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Chamwino, Dkt. Abdul Pumzi amesema uhitaji wa damu katika hospitali zetu nchini ni mkubwa mno, hivyo amewapongeza watumishi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kujitoa kwao kwa kuchangia damu kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *