NAIBU WAZIRI WA MADINI AKUTANA NA KAMPUNI YA NOBLE HELIUM INAYOTAFITI GESI

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amekutana na kuzungumza na Meneja wa Kampuni ya Noble Helium Joseph Uisso inayofanya utafiti wa gesi ya Helium katika maeneo ya Bonde la Ziwa Rukwa, Eyasi, Nyasa na Manyara.

Dkt. Kiruswa amekutana nao leo Juni 2022, katika kikao kifupi kilichofanyika katika ukumbi wa wizara Jijini Dodoma.

Katika kikao hicho, Dkt. Kiruswa na uongozi wa Kampuni ya Noble Helium wamezungumzia kuhusu maendeleo ya shughuli za utafiti zinazoendelea katika maeneo hayo. Aidha ameahidi kushughulikia changamoto zote walizonazo mapema.

Zifuatazo ni picha mbalimbali za kikao hicho kifupi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *