Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Kampuni ya Ranchi za Taifa NARCO Mhandisi Cyprian Luhemeja amesikitishwa na Kampuni hiyo kusema kuwa haina Fedha na kuahidi kwenda kufanya Mageuzi makubwa.
Mhandisi Luhemeja ameyasema hayo leo Juni 20, 2022 Jijini Dodoma wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa NARCO ambapo Mgeni Rasmi akiwa ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki
amesema kitendo cha Narco kusema haina fedha huo ni mtizamo wa fikra kwani tatizo sio Pesa bali ni mawazo
Ameahidi kuwa ndani ya Siku 100 atakaa na Bodi na kuhakikisha wanafanya mabadiliko makubwa
“NARCO imedumaa kwa sababu nyimgi, na watanzania watusamehe sana na Mheshimiwa Waziri utusamehe sana haya ni makosa makubwa”
Ameeleza kuwa Narco inapaswa kuwa Daraja kati yake na Wafugaji wa kawaida na kuwa kielelezo cha ufugaji nchini
“Watu wanafuga ng’ombe lakini hawajivunii ufugaji wao, mtu ana ng’ombe zaidi ya mia mbili lakini anaogopa kuwauza kwa sababu hajui anauza wapi.Mwaka jana tumekumbana na changamoto ya ukame.wafugaji wote walikimbia Mto Ruvu kwa sababu ya kutafuta malisho jambo ambalo ni Makosa ya Narco”
Luhemeja amefafanua kuwa Kampuni hiyo inapaswa kutoka mbele na kuuza Biashara zao ili wananchi waweze kuuza ng’ombe kwani Wafugaji hawawezi kutabiri soko la Biashara
Amesisitiza jambo hilo haliwezekani na ni hatari kwani hata Narco wanatumia Macho kununua bidhaa
“Tutatengeneza Bei elekezi ya kilo ya ng’ombe akiwa katika uhai wake ili wananchi watabiri kwamba mwaka huu ninapouza ng’ombe napewa Shilingi fulani na haya tunatakiwa yafanyike haraka sana”
Aidha, ameahidi kwenda kufumua muundo wa NARCO na kuanza upya ili kila Mkoa kuwa na Ranchi pia na Meneja wa Mkoa na kuachana na kujiendesha kijadi.
Akizungumzia kuhusu Soko la Nyama Mwenyekiti Luhemeja amesema nalo pia linapaswa kwenda kuangaliwa ili wananchi waweze kuridhika.
“Kesho tuna Kikao cha Bodi cha Kwanza, Menejimenti leo msilale, tunataka mtuletee Ripoti zote za Viongozi”
Amemuhakikishia Waziri wa Mifugo kuwa Narco itakuwa kielelezo na itaratibu wafugaji kwani Kazi kubwa itafanyika
Kwa upande mwingine amemshukuru Rais Samia kwa imani kubwa aliyompa kwa Kumteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NARCO