
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa ameshiriki Kikao cha tano cha Kamati kuu ya Taifa ya Sensa na Watu na Makazi ya mwaka 2022 na Tukio la kukabidhi taarifa ya utekelezaji wa oparesheni anwani za makazi.
Kikao hicho kimeongozwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na kuhudhuliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdullah pamoja na Mawaziri na viongozi mbalimbali wa kisekta katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Dar es salaaam. Leo Juni 18,2022.




