WAZIRI AWESO: KILA MMOJA ANA NAFASI YAKE NA MCHANGO WAKE KATIKA MAISHA

Katika kuitafsiri kwa usahihi dhana ya Uongozi bora, Waziri wa Maji Jumaa aweso kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Juni 17, 2022 ameweka chapisho la picha lililoambatana na ujumbe muhimu wa kwa Watumishi wake wanaohudumu katika sekta ya usafirishaji mara baada ya kufanya kikao nao.

Waziri aweso amesema “Nimepata baraka ya ugeni wa uwakilishi wa madereva wetu wa Wizara ya Maji ofisi ndogo Dodoma ikiwa ni timizo la mihadi yetu ya kuonana na kusemezana ikiwa ni pamoja na dhamira yangu ya kuwapongeza na kutambua mchango wao kwa Wizara yetu,
Sekta yetu inahitaji sana ufuatiliaji na usimamizi na ina upekee wa aina yake”

“Watumishi wenzetu hawa wamekua sehemu ya kufanikisha safari zetu za kila wakati na kutufanya kufanikisha malengo, kwa hili niseme wazi tunawathamini sana na tunawashukuru kwa nafasi yao na kutimiza wajibu wao.”-Waziri Aweso

“Mwisho nimewashauri na kuwachangia katika kuhakikisha wanakua na mfuko mahususi wa kusaidiana na kushirikiana.
Imani yangu ni kwamba, kila mmoja ana nafasi yake na mchango wake katika maisha ya kazi na maisha ya kila siku.”-Waziri Aweso

cc-jumaa_aweso instagram

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *